Thursday, August 30, 2012

Sasa unaweza kusikiliza baadhi ya Radio za Bongo live online

Ili kuepukana na tabu ya kujua links na websites (tovuti) ya baadhi ya radio zinazorusha matangazo online moja kwa moja (live) blogu hii imeanza kukusanya baadhi ya links hizo ambazo utasikiliza radio hizo live kwa kusikiliza vipindi vinavyoendelea muda wote. 

 Hizi ni jitahada za kufikishiana habari hata kwa wale waliopo nje ya mawimbi ya matangazo ya radio husika na pia kuwasaidia waliopo maofisini wasio na radio au simu za kusikilizia Radio. 

Kumbuka Radio hizi zitasikilizwa moja kwa moja kupitia tovuti zao husika hivyo unashauriwa kutunza anuani zao pindi utakapozipata kupitia blogu hii ili uweze kuzikiliza muda wote upendao.

Baadhi  ya radio hizo ni BBC idhaa ya kiswahili, Radio Free Africa, Kiss Fm na Clouds Fm. Jitahada za kutafuta  (Viunganisho) links nyingine zinaendelea. Tazama upande wa kulia wa  blogu hii kuzisikilza.

Wednesday, August 29, 2012

UDSM yatoa namba za Wanafunzi wenye matatizo na matokeo yao

Chuo Kikuu cha Dar-es- salaam (UDSM) leo kimetoa namba za wanafunzi ambazo zina matatizo na matokeo yao ikiwemo matatizo ya Supplimentary, Discontinuation from studies na mitihani maalumu (Special examinations)

Tangazo hiliu ni la msingi sana kwa wanafunzi wote waliohitimu na wanaoendelea na masomo UDSM. Tafadhari ukipata taarifa hii mjulishe na mwenzio uokoe jahazi. Kumbuka, namba hizi na matatizo hayo hayatofautiani na yale yanayopatikana kwenye akaunti za ARIS za wanafunzi husika.

Tarehe maalumu ya kuanza Supplimentary na special exams ni 24 septemba 2012.

"Ukitaka kujua hatima yako bofya hapa"

Monday, August 27, 2012

Changamkia nafasi za kazi UDOM

Chuo Kikuu cha Dodoma kimetoa nafasi mbalimbali za kazi katika tovuti yao. Kazi hizo zimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni kazi za kiutawala (Administrative ones) na za kitaaluma (academic ones). Katika kazi hizo kwenye administraive ones utakutana na nafasi mbalimbali za kazi na za kada tofauti kama mtendaji ofisini na katika kundi la academic ones utakuta kazi za kufundisha kama mtaaluma.

Ni wakati wako kijana kuchangamkia dili hizo. Tarehe ya mwisho kupokea maombi ni tarehe 10 september 2012. Wahi kabla ya jahazi kuzama.