Tuesday, July 10, 2012
Wednesday, July 4, 2012
Tumehitimu Vyuo Vikuu……….. wapi ajira?
Mwishoni mwa mwezi wa sita na mwezi huu wa saba taasisi nyingi
za elimu ya juu zimeanza kutoa wahitimu wa taaluma mbalimbali na katika ngazi tofauti za elimu toka cheti, diploma,
degree na masters. Wanafunzi tuliohitimu ni maelfu kwa maelfu kutoka zaidi Vyuo
vikuu 30 na Vyuo vya mafunzo ya ufundi
(Vocational Training Colleges). Kundi lote hili la wahitimu linahitaji ajira
katika makampuni binafsi na Serikali huku asilimia ndogo sana ya wahitimu wakipanga
kujiajiri.
![]() |
Baadhi ya Wahitimu wa Shahada ya Sayansi Siasa na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam 2009/12 katika picha pamoja baada ya mtihani wao wa mwisho. Picha kwa msaada wa Political Science gradutes 2012 facebook page |
Inafahamika wazi kuwa mwajiri mkuu nchini ni
Serikali huku sekta binafsi ikichikua asilimia zilizobaki. Pia ifahamike kuwa
hata hao waajiriwa katika sekta binafsi hufanya kazi mara nyingi katika sekta
isiyo rasmi (informal sectors). Wakati jamii kubwa ikitegemea Serikali itoe
ajira kwa wahitimu hawa, Serikali yenyewe imejikuta ikishindwa hata kuwahudumia
watumishi waliopo. Matatizo mengi yanayohusu ajira za wafanyakazi wa Serikali yameshuhudiwa
kwa muda mrefu likiwemo hili linaloshika Vichwa vya habari hivi sasa la mgomo
wa madaktari. Serikali imeshindwa kutoa stahili husika kwa Wafanyakazi wake.
Pia serkali imeweka vigezo vigumu sana
ambavyo kwa wahitimu wa sasa na wa mwaka jana hawawezi kuomba kazi. Moja ya
vigezo hivyo ni kuwa na cheti halisi cha chuo Kikuu na si Provisional
statements au transcripts kama ilivyozoeleka. Pili uzoefu kazini bado ni wimbo
usiochuja, bado uzoefu usiopungua miaka kadhaa unasisitizwa. Jambo jingine ni
ufinyu wa bajeti ya serikali katika kuongeza ajira. Serikali imekua ikijitetea
kuwa haina uwezo kifedha kuajiri idadi kubwa ya Wafanyakazi licha ya kuwa na upungufu
mkubwa wa watumishi katika taasisi zake. Jingine ni unamfahamu nani kwenye
system ya Serikali ili upate kazi kama humfahamu mtu basi nauli yako imeisha. Je
kama hali ndo hiyo maelfu ya wahitimu mwaka huu tutaende wapi?
Kwa upande wa Sekta binafsi, makampuni mengi hayaajiri idadi kubwa ya watu
kwa misingi ya kupunguza gharama za uendeshaji. Idadi ndogo sana ya wahitimu
huajiriwa na Sekta binafsi iliyo rasmi kama Benki, Viwandani na Makampuni
madogomadogo ya biashara. Pia ifahamike tena kuwa sekta binafsi huchagua kundi Fulani
la Wahitimu hasa kwa kuangalia ufaulu na uzoefu kazini. Kwa wahitimu waliowengi
uzoefu bado mdogo zaidi ya mafunzo ya vitendo ambayo hupatikana kwa njia ya
interns (Practical trainings). Kwa upande wa performance kuna kundi kubwa la
wahitimu halina First Class degrees au diploma wanazotaka. Uzito na ugumu wa
kozi vimetofautiana kutoka aina Fulani ya masomo kama engineering Vs arts au
toka Chuo kimoja hadi kingine kama University of Dar es Salaam Vs Tumaini n.k.
Kwa utofauti huu wangapi wataajiriwa?
Kwa upande wa Kujiajiri bado kuna tatizo
kubwa. Ni idadi ndogo sana ya wahitimu ambao wana uwezo wa kujiajiri wenyewe. Tatizo
sio kuwa hawana uwezo wa kujiajiri kwa kufanya biashara na mambo mengi bali
ukata wa kifedha na mfumo wa elimu ni vyanzo vikuu hali hii. Mfumo wa elimu ya
bongo unamuandaa mwanafunzi kuajiriwa na si kujiajiri. Mfano mzuri ni pale mtu
aliyehitimu VETA anapotafuta ajira. Mfumo huu hauna utofauti na ule wakikoloni
wa kuandaa watu kufanya kazi za kuajiriwa maalufu kama white Color Jobs. Jambo jingine
ni kukosa kwa mtaji wa kuanzisha biashara. Benki zimekuwa na imani ndogo sana
kukopeha wahitimu kwa kuwa hawana dhamana yoyote zaidi ya Cheti na akili tu
kichwani. Pia wengine wanakatishwa tama na
urasmu wa kusajiri biashara Serikalini na mfumo mzima wa kodi ambao unaharibiwa
na wafanyakazi wenye tabia ya rushwarushwa (rent seeking behavior)
![]() |
Mimi wa pili kushoto waliosimama na wahitimu wengine baada ya kumaliza mtihani wa mwisho wa shahada ya Sayansi ya Siasa na Utawala, June 20, 2012 Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) |
Hii ndio halisi ambayo wahitimu wengi wa Vyuo
mbalimbali nnchini wanakumbana nazo. Jamii haitakiwi kuwalumu Vijana kwa dalili
za utegemezi wanaouonyesha zaidi jitahada malimu zinahitajika kutatua tatizo la
kupunguza vifaranga vingi vinavyototolewa Vyuo Vikuu huku vikienda kwenye
mabanda ya no ajira.
Tujifunze kupitia haya. Tutafute njia mbadala
wa kutatua tatizo kwa kila mdau nchini.
Monday, July 2, 2012
Tuendelee kuitafakari Bajeti ya Serikali 2012/13
Kupata bajeti kuu ya Serikali, Wizara pamoja na bajeti vivuli kwa ajili ya tafakari "bofya hapa"
Happy Birthday!
Umetimia mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa blog hii, ilikua
ni july 2011 na sasa ni july 2012. Yapo malengo mengi ambayo hayajatimizwa kama
ilivyopangwa hapo awali. Lakini huo si mwisho wa kuifanya Blog hii kuwa bora
zaidi na yenye chambuzi na habari za kina.
Ni dhahiri
kwamba kushindwa kufikia malengo kwa asilimia mia ni moja ya dalili za
kushindwa kutimiza mipango. Hata hivyo kushidwa kutimiza lengo ni changamoto
kwangu, kunanipa nguvu ya kujipanga zaidi na kuandaa mipango ya muda mfupi na mrefu ili kutimiza lengo.
Napenda kuwashukuru wasomaji na wachangiaji wote kwa
kushiriki katika Blog hii. Pia shukrani za dhati ziwaendee wote ambao kwa namna
moja au nyingine wamesaidia kuwapo kwa blog hii. Napenda tuungane wote kutimiza
malengo kwa kuchangia habari na maoni mbalimbali ambayo yatakua chachu ya
maendeleo ya jamii yetu ya Tanzania.
Napenda niahidi kuwa sasa Blog hii itakuwa na taarifa
za wakati kwa kushirikiana na viunganishi vingine vya chambuzi na habari. Hii ni
moja ya njia ya kuzikusanya habari na chambuzi mbalimbali sehemu moja. Hii itasaidia
kujifunza mengi kwa wakati. Tafadhari tusichoke kufuatilia Blog hii katika
masuala yote ya siasa, uchumi, jamii, elimu, Sayansi na teknolojia na burudani.
Karibuni sana na msikose kuisoma Blog hii kila siku.
Nuzulack J. Dausen
Subscribe to:
Posts (Atom)