Nuzulack Dausen
Kifo cha
Msanii wa Maigizo na Muziki Hussein Mkiety a.k.a Sharo Milionea kimenishtua
sana. Nilipoipata habari ya kifo chake mapema leo asubuhi nilidhani rafiki
zangu wananitania kwa kuwa msanii huyu alikuwa ni maarufu wa vituko na vichekesho vingi na
alishika akili za watanzania wengi kwa staili yake ya Kisharobaro hivyo
walitaka tu kunighiribu akili yangu.

Binafsi nautambua
mchango wa Sharo Milionea katika gemu la Bongo Movies na Bongo Fleva. Uwepo wa
Sharo Milionea katika gemu kwa muda mfupi kuliamsha ari ya wasanii wengi
wachanga kuingia kwenye gemu na hata wale wakubwa kukaza ili kukabilana na
ushindani mkubwa alokuwa ameuanzisha Sharo Milionea.
Kwa muda huo
mfupi katika muziki na filamu Sharo amekuwa gumzo miongoni mwa wadau wa muziki
na filamu kwa staili zake ambazo zimekua zikitoa burudani safi ya tofauti na
wasanii wengine.
“Umebugi
meeni” “nasubiri mrija meeni” ni baadhi tu ya maneno ya Sharo yaliyozoeleka
midomoni mwa mashabiki wake. Maneno hayo hayakumpa tu umaarufu yemwenyewe bali
mpaka baadhi ya bendi za Dansi ziliyatumia. Watoto mitaani na baadhi ya watu
wazima walitumia maneno hayo kutaniana.
Binafsi
nimesikitishwa sana na kifo chake lakini hatuna cha kufanya kwa kuwa yote hayo
ni mipango ya Mungu. Yeye ametangulia, sisi tutafuatia.
Nawapa
pole ndugu wa karibu wa marehemu Sharo Milionea, Wasanii wote wa Bongo Movies
na Bongo Fleva, Mashabiki na Watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na Msanii
muhimu sana katika maendeleo ya sanaa nchini.
Bwana
ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Mungu amlaze mahali pema peponi
Sharo Milionea.
No comments:
Post a Comment