Nuzulack Dausen
Wakandarasi
na wafanyabiashara mbalimbali nchini wanatarajia kunufaika na mkopo wa mashine
na mitambo mbalimbali ya Ujenzi ya aina ya Caterpillar baada ya Benki ya
Stanbic Tanzania kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya Cat
Financial ambayo ni mdhamini mkuu wa kifedha wa Vifaa hivyo.
Katika
mkataba huo Wakandarasi wa ndani watanufaika na huduma za kifedha hasa zile za
mikopo zenye masharti nafuu na zitakazowawezesha kununua mitambao bora, ambayo
itasaidia utendaji kazi kwa ufanisi na ubora zaidi.
 |
Lilian Kitomari(kushoto) wa Stanbic Benki akizungumza wakati wa hafla hiyo, katikati ni Neimat El Maghraby Mkuu wa Kitengo cha fedha Mantrac Unatrac Group na kulia ni Adel Selim meneja wa mantrac Kanda ya Afrika Mashariki. |
Akizugumza
katika hafla ya kusainiana mkataba huo jijini Dar es salaam hivi karibuni Meneja
wa Rasilimali na Bima wa Benki ya Stanbic Tanzania Lilian Kitomari alisema
benki yake itaendelea kutoa huduma na njia madhubuti zitakazosaidia wateja wake
kutatua matatizo mbalimbali ya kifedha ili kukuza biashara zao nchi nzima.
 |
Meneja wa Mantrac kanda ya Afrika Mashariki Adel Selim akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano ya kibiashara yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam. |
Aidha, Rais
wa kampuni ya Cat Financial ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Caterpillar Inc,
Kent Adams, alisema kuwa “mchanganyiko huo wa bidhaa unaotambuliwa kimataifa
kati ya kampuni ya Cat na Benki ya
Stanbic ambazo zinaheshimiwa na kuaminiwa na taasisi za kifedha barani Afrika
vitajenga nguvu ya ushindani wenye faida kwa mitandao yetu na wateja wao na
kuongeza mauzo yao ya vifaa.”
Naye Naibu
Ofisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Standard, Bw. Ben Kruger, alisema “tuna thamini
uhusiano wetu uliopo na kampuni ya Cat na tunaamini kuwa uhusiano huu unatoa
jukwaa la kuimarisha mahusiano haya na kutoa huduma zaidi kwa nchi nyingine
katika bara la Afrika.”
Alisema kuwa
Benki ya Standard Chertered ambayo ni
Kampuni mama ya Stanbic Tanzania yenye shughuli zake barani Afrika ina timu ya
wataalam ambao ni wazoefu wa biashara na
kanuni, watahakikisha upatikanaji wa huduma bora kwa wateja wa benki hiyo na
kampuni ya CAT Financial.
Aliongeza
kuwa mpango huo wa magari na rasilimali unafadhiliwa na Benki ya Standard Chartered ya Afrika Kusini.
Wafanyabiashara
hao wa Tanzania wataungana na wenzao wa nchi tano za Nigeria, Kenya Uganda,
Ghana na Sierra Leone, ambapo huduma hizo zitatolewa.
Ni kipindi
kirefu sasa Wakandarasi wengi nchini
wamekuwa wakilalamikia kukosa mitaji itakayowawezesha kununua mitambo mikubwa
na bora ambayo ni chachu ya kufanya kazi
zao kwa ufanisi na ubora zaidi jambo linalowafanya kukosa zabuni mbalimbali za
Ujenzi ambazo kampuni za kigeni zimekuwa zikinufaika nazo kwa kuwa na mitambo
na mashine za kisasa.