Saturday, December 1, 2012

ANAOMBA MSAADA WA KUSOMESHWA



Nuzulack Dausen

MKAZI wa Tabata Kisukuru Jijini Dar es salaam Mahamoud Said (22) (pichani juu) anawaomba Wasamaria wema kokote nchini kumsaidia msaada wa fedha zitakazomsaidia kumalizia  gharama za masomo  yake.

Said ni mlemavu wa mkono asiyejiweza ambaye amefanikiwa kupata udahili wa masomo ngazi ya cheti katika Chuo cha Utumishi wa Umma Kilichopo Jijini Tanga lakini ameshindwa kujiunga mapema na Chuo hicho baada kukosa fedha.

Anasema kuwa alipata ulemavu wa mkono mwaka 1998 wakati akicheza mpira ambapo miaka miwili baadaye ulianza kutoa funza ndipo daktari aliamuru mkono huo kukatwa ili kumnusuru maisha yake.
Ombi hilo linakuja baada ya kupata msaada wa ada kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision ambalo lilimsaidia kiasi cha Shilingi laki nane ambayo inatosheleza kulipia karo kwa mwaka mmoja tu. 

Kiwango hicho kilichobaki kinanajumuisha  fedha za kujikimu, nauli, sare, vifaa vya kusomea pamoja na michango yote ya Chuoni.

Awali habari ya kuomba msaada huo ziliandikwa kwenye gazeti la Mwananchi tarehe 27 Novemba mwaka huu kuhusu ombi la msaada wa kusomeshwa masomo hayo lakini kwa bahati mbaya hakuna aliyejitokeza kumsaidia, hata hivyo anawaomba wasamaria wema kujitolea ili aweze kufanikisha masomo yake.

Yeyote mwenye mapenzi mema na mwenye nia ya kumsaidia tafadhari apige simu au achangie  kupitia M-pesa namba 0766 469 548 au Tigo Pesa namba 0717 511 295.

Friday, November 30, 2012

UKUAJI WA UCHUMI NCHINI HAUTAWASADIA WATANZANIA-WADAU




UKUAJI wa uchumi nchini hautawasaidia  watanzania kutoka kwenye lindi la umaskini iwapo njia mbadala  hazitachukuliwa kudhibiti rushwa na  uhusiano usiosawia  baina ya serikali na sekta binafsi, imeelezwa.

Wakichangia mada kuhusu wajibu  wa sekta binafsi katika kupunguza umaskini Jijini Dar es salaam juzi, wadau mbalimbali wa maendeleo walisema kuwa jitahada za Tanzania kukuza uchumi wake hazitakuwa na msaada wowote kwa Watanzania katika kupunguza umaskini iwapo rushwa na  uhusiano hasi baina ya Serikali na sekta binafsi havitaondolewa.

Walisema kuwa uhusiano uliopo baina ya Serikali na sekta binafsi hauna usawa kwani sekta binafsi imekuwa na nguvu nyingi kuliko Serikali na kusababisha malengo na jitaha za  Serikali kupunguza umaskini nchini kutofikiwa ipasavyo.

Mwendesha Walsha ya kujadili wajibu wa Sekta binafsi katika jitahada za kupunguza umaskini Bakari Bujari (kushoto0 akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa British Council Dkt Conor Snowden wakati wa uzinduzi wa Walsha hiyo Jijini Dar es salaam juzi.
Akizungumza katika mdahalo huo Afisa Mtendaji wa Taasisi ya kimataifa  isiyo ya Kiserikali ya  VSO  Marg Mayne alisema kuwa taarifa ya Benki ya Dunia inaonyesha Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi lakini ukuaji huo umeshindwa kuwakomboa Watanzania wengi hususani waishio vijijini kutoka kwenye lindi la umaskini bali umeongeza tofauti kati ya maskini na matajiri.

Aliongeza kuwa ugunduzi wa gesi na mafuta nchini unaotarajia kukuza uchumi wa nchi kwa aslimia 6.5 hadi 7 hautaleta mabadiliko yoyote iwapo mfumo wa sasa wa uhusiano baina ya serikali na sekta binafsi hautavunjwa.
Alishauri uanzishwaji wa ushirikiano wa kina na ushawishi uliosawa baina ya wadau wa maendeleo na sekta binafsi ambao utaenda mbele zaidi ya sera ya Wajibu wa kampuni kwa jamii (CSR) ili kuongeza mchango mkubwa wa makampuni katika jitahada za kupambana na kupunguza umaskini nchini.

Rananie Kunanayagam, Mkuu wa Utendaji wa Jamii Kampuni ya BG group alisema ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi si jambo jipya duniani kwani lilishakuwepo miaka 15 hadi 20 iliyopita katika nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania lakini umaskini bado upo palepale hivyo anahitajika mtu wa kusimamia uhusianobaina  ya Serikali na sekta binafsi.
“Kunahitajika uwepo wa mtu au taasisi katikati ya Serikali na Sekta binafsi ambaye hatang’ata upande wowote na kuwashawishi wote kutekeleza majukumu yao kwa usahihi” alibainisha Kunanayagam.

Mshiriki wa mdahalo wa kujadili wajibu wa Sekta binafsi katika jitahada za kupunguza umaskini nchini akitoa maoni juu ya mada hiyo juzi katika ukumbi wa British Council.Jijini Dar es salaam juzi.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Phillipe Poinsot alisema kuwa lazima kuwe na mgawanyo sawa wa wajibu baina ya Serikali na sekta binafsi katika kupambana na umaskini na pia Serikali izidishe uhusiano ndani ya Sekta binafsi.

Alisema kuwa Serikali ihakikishe inatengeneza miundombinu na mazingira rafiki kwa sekta binafsi kwa kutengeneza barabara safi, umeme wa uhakika, sheria thabiti, usimamizi mzuri wa rasilimali,  wasomi na viongozi  makini wasiopenda rushwa wakati huohuo  sekta binafsi ina wajibu wa kutoa kodi halali, uwazi katika uendeshaji, kuendeleza teknolojia na kutoa ajira stahiki kwa Watanzania.

Mjumbe wa Mdahalo huo Semkai Kilonzo alisema uwepo wa miongozo mingi inayohusika na jitahada za kupunguza na kupambana na umaskini kama MKUKUTA, Dira ya 2025, Kilimo Kwanza na mingine ni chanzo kikubwa cha ukuaji wa uchumi nchini kushindwa kuwakomboa Watanzania kutoka kwenye lindi la umaskini.
“Uwepo wa Miongozo mingi kwa wakati mmoja  kama MKUKUTA, Mkurabita, Kilimo Kwanza kunachanganya Wadau wa maendeleo na pia imekuwa haina ushirikishwaji wa Wananchi katika kufanya maamuzi ya maendeleo yao hivyo inashindwa kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau” alisema Kilonzo.

Mdahalo huo Uliandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya VSO International ikishirikana na BG Tanzania na British Council ambapo wadau walitaka rushwa itokomezwe,  uwazi wa utendaji katika makampuni na serikali, kuanzishwa kwa sera na sheria inayotoa kiwango na aina za miradi inayoweza kufanywa na makampuni katika Sera ya Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR).




Tuesday, November 27, 2012

FASTJET YAZINDUA RASMI SAFARI ZA NDEGE MIKOANI



KAMPUNI ya ndege ya Fastjet  imezindua rasmi safari zake nchini katika Mikoa mitatu ya Dar es salaam, Mwanza na Kilimanjaro kwa safari mbili za kila siku Dar-Mwanza na Dar-Kilimanjaro na ndege aina ya Airbus A319.  

Afisa Mtendaji wa Fastjet Ed Winter kushoto akiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba wakati wa uzinduzi wa safari ndege za kampuni hiyo.
Akizungumza katika Uzinduzi huo leo Jijini Dar es salaam mgeni rasmi Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba alisema kuwa kuanza kwa safari za ndege za kampuni hiyo inayotoa huduma hiyo kwa bei rahisi kutachangia ukuajiw auchumi kwa kasi sana kwa kuongeza idadi ya Watalii, kutaongeza mzunguko wa biashara na pia kurahisisha safari binafsi za Watanzania.

Tizeba alisema kuwa Serikali inawaunga mkono sekta binafsi hususani katika usafirishaji wa naga kwa kurekebisha Viwanja vilivyopo na kuendelea kuvitengeneza vipya kikiewemo cha Songwe Mbeya kinachotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi desemba Mwaka huu. Aliongeza kuwa kwa sasa wanarekebisha Viwanja Vya Tabora, Kigoma na Mafia huku Kiwanja ch mpada kikiwa kimezinduliwa hivi karibuni.

 Hata hivyo aliitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini(TAA) kuhakiksha inarekebisha miundombinu na huduma za Viwanja vya Mwanza na Kilimanjaro ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya wasafiri watakaotumia Viwanja hivyo.

 Afisa Mtendaji wa Kampuni hiyo Edward Winter alisema kuwa Kampuni yake ina uzoefu mkubwa kufanya biashara hiyo kwa bei nafuu hivyo watanzania wasihofie kushindwa kuendelea kwa kampuni hiyo na kuongez kuwa Safari nyingi zaidi zitaongezwa katika nchi nne za afrika za Kenya, Ghana, Rwanda na Angola.

 Aliongeza kuwa huduma zinazotolewa katika ndege hiyo ni za kisasa na zinazokidhi viwango vya Kimataifa vikiwemo viwango vya Ulaya (European Airline Standards). Hivyo basi Watanzania wachacharikie huduma hiyo ya haraka na bei rahisi kutokea nchini.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Fastjet.

Afisa Mtendaji wa Fastjet Ed Winter akihutubia wadau wakati wa uzinduzi wa safari za  ndege za Kampuni hiyo.

Airbus A319 ya Kampuni ya Fastjet katika picha kabla ya safari ya Uzinduzi mapema leo asubuhi

Maofisa wa Fastjet wakijadilaiana kabla ya ndege Airbus A319 kufanya safari ya Uzinduzi Jijini Dar es salaam

Waandishi wa Habari wakipata maelezo kuhusu safari za ndege za Kampuni ya Fastjet.


Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba kushoto akipewa maelekezo  juu ya ndege ya Airbus A319

Wahudumu wa Fastjet wakiwa katika pozi wakati wa uzinduzi huo.
Safari za ndege hizo zinatarajiwa kuanza mapema keshokutwa Alhamisi ya tarehe 29 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam na gharma yake kuwa ya chini sana ya sh 32000 kwa sfari moja bila kodi sawa na dola 20 za Kimarekani. Hata hivyo gharama za safari hizo zinabadilika pindi muda wa kusafiri unapokaribia.
Hivi ni baadhi ya vitafunwa vinavyopatikana ndani ya ndege ya Fastjet Airbus A319

Watanzania wamehimizwa kuwahi kukata tiketi ili kupata huduma hiyo kwa bei nafuu sana kwani kuchelewa kukata tiketi kutaongeza kiwango cha nauli.