Thursday, August 30, 2012

Sasa unaweza kusikiliza baadhi ya Radio za Bongo live online

Ili kuepukana na tabu ya kujua links na websites (tovuti) ya baadhi ya radio zinazorusha matangazo online moja kwa moja (live) blogu hii imeanza kukusanya baadhi ya links hizo ambazo utasikiliza radio hizo live kwa kusikiliza vipindi vinavyoendelea muda wote. 

 Hizi ni jitahada za kufikishiana habari hata kwa wale waliopo nje ya mawimbi ya matangazo ya radio husika na pia kuwasaidia waliopo maofisini wasio na radio au simu za kusikilizia Radio. 

Kumbuka Radio hizi zitasikilizwa moja kwa moja kupitia tovuti zao husika hivyo unashauriwa kutunza anuani zao pindi utakapozipata kupitia blogu hii ili uweze kuzikiliza muda wote upendao.

Baadhi  ya radio hizo ni BBC idhaa ya kiswahili, Radio Free Africa, Kiss Fm na Clouds Fm. Jitahada za kutafuta  (Viunganisho) links nyingine zinaendelea. Tazama upande wa kulia wa  blogu hii kuzisikilza.

No comments:

Post a Comment