Friday, December 28, 2012

HERI YA MWAKA MPYA 2013

 
NDUGU mpenzi msomaji napenda nichukue nafasi hii adhimu kukutakia Heri ya mwaka mpya 2013 wenye mafanikio tele yasiyo na kifani.

Pia napenda nikupongeze kwa kufanikiwa kuumaliza mwaka salama licha ya kuwa ulipata changamoto za hapa na pale, usijali hiyo ni sehemu ya maisha ambayo binadamu tumeumbiwa.

Mungu akubariki na endelea kusoma kila siku Blog hii mara uingiapo mtandaoni.
 

HAPPY NEW YEAR 2013.

Thursday, December 27, 2012

TAARIFA YA MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO JOHN MNYIKA KWA VYOMBO VYA HABARI


Nakusudia kutumia kifungu cha 10 cha Sheria
ya ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kutaka nakala ya mkataba wa mkopo wa masharti kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.225 (shilingi trilioni 1.86) kutoka China.

Nitataka pia nakala za mikataba wa mradi wa miundombinu ya gesi asilia ambayo itahusisha ujenzi wa mitambo ya kusafishia gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara na ujenzi wa bomba kuu la kusafirishia gesi asilia la inchi 36 kutoka Mtwara kupitia Lindi, Pwani hadi Dar es Salaam lenye umbali wa kilometa 532.

Hii ni kwa sababu mpaka sasa Wizara ya Nishati na Madini haijatekeleza pendekezo nililowasilisha bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwamba kutokana na unyeti wa mradi huo kwa mustakabali wa nchi na maisha ya wananchi wa sasa na baadaye Serikali ilipaswa kuwasilisha bungeni na kuweka wazi kwa umma mkataba wa mradi husika.

Pendekezo hilo lingeliwezesha Bunge kuishauri na kuisimamia serikali kuanzia katika hatua za awali kuhakikisha kwamba maslahi ya taifa yanalindwa katika hatua zote na pia wananchi wananufaika kutokana na fursa za uwekezaji huo mkubwa.

Kutokana na Serikali kutokuzingatia pendekezo hilo na badala yake Rais Jakaya Kikwete kufanya uzinduzi wa mradi huo tarehe 8 Novemba 2012 Mkoani Dar es salaam huku usiri ukiendelezwa malalamiko yameanza kujitokeza katika maeneo ya mradi husika hususan katika Mkoa wa Mtwara.

Aidha, Serikali irejee katika mapendekezo niliyotoa bungeni na kutoa maelezo kwa umma ya sababu za bomba hilo kujengwa kutoka Mtwara mpaka Dar es salaam na kueleza kwa uwazi manufaa ya mradi huo na miradi mingine inayopaswa kutekelezwa katika mikoa ya Kusini kwa maendeleo ya wananchi husika.

Tarehe 27 Julai 2012 nilieleza bungeni kuwa pamoja na ujenzi wa mitambo miwili ya kusafishia gesi asili Mnazi Bay na Songo Songo kama sehemu ya mradi huo; Serikali inapaswa kueleza ni miradi ipi inayoambatana na mradi huo ambayo imepangwa kuwanufaisha wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara ikiwemo kuharakisha utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa MW 300 Mtwara na MW 230 wa Somanga Fungu (Kilwa).

Kwa upande mwingine, utekelezaji wa mradi huo unaendelea bila kuwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo ingepaswa kuishauri na kuisimamia Serikali hivyo ni muhimu Spika wa Bunge akachukua hatua kutokana na barua niliyomwandikia mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2012 ambayo mpaka sasa haijajibiwa.


Ikumbukwe kwamba katika barua hiyo nilitoa mwito kwa Spika atumie madaraka na mamlaka yake kutangaza kwa umma kamati nyingine ya kudumu ya Bunge itayoshughulikia nishati na madini ikiwemo masuala ya gesi asili kwa sasa kufuatia hali tete na tata kuhusu sekta ndogo ya gesi asilia nchini na kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.

Pamoja na mambo mengine nilipendekeza Spika aelekeze kamati hiyo kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge ya mwaka 2011 kuhusu Sekta Ndogo ya Gesi Asili ikiwemo juu ya hatua iliyofikiwa katika kushughulikia tuhuma za ufisadi, madai ya mapunjo ya fedha za mauzo ya Gesi asili na hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya sera, mpango mkakati na sheria ya gesi asili.

Hatua hii ni muhimu kwa sasa kwa kuwa hata baada ya uamuzi wake kuhusu tuhuma za rushwa kwa wajumbe wa Kamati husika, Spika hakueleza hatma ya Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa hali ambayo imeacha ombwe la uongozi na usimamizi wa kibunge (Parliamentary Oversight) kwenye sekta hizi nyeti kwa uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
26/12/2012
Taarifa hii pia inapatikana kwemye ukurasa wake wa Facebook wa John Mnyika.

Sunday, December 9, 2012

DK. BILAL AZINDUA DHL HOUSE

Na Nuzulack Dausen

Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal mwishoni mwa wiki iliyopita alizindua rasmi jengo  la kuhifadhia mizigo na ofisi za kampuni  ya DHL Express (DHL House)  lilopo ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikiwa ni moja za jitahada za kampuni hiyo kurahisa na kuongeza ufanisi katika usafirishaji wa mizigo ya nje na ndani ya nchi.

Akizindua jengo hilo Dk Bilal alisema ujenzi wa jengo hilo unaonyesha wazi kuwa DHL imepania kuboresha huduma zake nchini kwa kusafirisha mizigo mingi na kuhudumia wafanyabiashara wengi zaidi kwa kwa wakati.
Alisema Serikali itaenedela kuboresha miundombinu ili kutengeneza mazingira rafiki kwa uwekezaji.

Aidha, Bilal aliwataka wawekezaji wote nchini kuiga mfano wa DHL wa kuajiri asilimia 99 ya wafanyakazi wazawa huku asilimia 40 kati yao wakiwa wanawake.

Alisema iwapo wawekezaji wataongeza imani kwa wazawa kwa kuwapa ajira basi tatizo la ajira linalolikumba taifa litatokemezwa na kuongeza kuwa wataalamu wazawa wapewe kipaumbele katika zabuni mbalimbali jambo litakalo ongeza tija kwa uchumi na maendeleo ya nchi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DHL nchini Braise De Souza alisema Kampuni yake itaendelea kuboresha huduma zake kwa kiwango cha juu na kuongeza kuwa wataendelea kuchangia masuala mbalimbali ya maendeleo ya kijamii kama kutunza mazingira, afya, elimu na kushughulikia masuala mbalimabali ya majanga ya dharura yanayolikumba taifa.

“Kazi yetu si usafirishaji pekee bali tunasghulikia pia na masuala ya kijamii kama kusaidia watoto hosptali ya Muhimbili, kutoa ajira kwa wanawake kwa asilimia nyingi zaidi, ma hivi karibuni tulidhamini tuzo ya Women of Determination iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu” alibainisha De Douza.

Sherehe hizo za Ufunguzi pia zilihudhuriwa na Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Suleiman Rashidi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said meck Sadiq na wakurugenzi
Viongozi wa Idara mbalimbali za DHL Express wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali waliohudhuria uzinduzi wa jengo la kuhifadhia mizigo na ofisi la DHL Express House.

Mshindi wa tuzo za Women of Determination Award Nusra Mohamed akiwa na Viongozi waliohudhuria uzinduzi wa DHL Express.

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akifungua rasmi jengo la DHL Express mwishoni mwa wiki. katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa DHL Blaise De Souza na kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe.

Mkurugenzi Mtendaji wa DHL Express( kushoto) akimpatia zawadi ya Kifaru Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal(katikati) na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa DSM Said Mecky Sadiq.

Dk Bilal akionyeshwa kitabu cha DHL EXpress na Mkurugenzi Mtendaji wa DHL Blaise De Souza.

Saturday, December 8, 2012

STANBIC NA CAT FINANCIAL WASHIRIKIANA KUKOPESHA WAKANDARASI



Nuzulack Dausen

Wakandarasi na wafanyabiashara mbalimbali nchini wanatarajia kunufaika na mkopo wa mashine na mitambo mbalimbali ya Ujenzi ya aina ya Caterpillar baada ya Benki ya Stanbic Tanzania kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya Cat Financial ambayo ni mdhamini mkuu wa kifedha wa Vifaa hivyo.

Katika mkataba huo Wakandarasi wa ndani watanufaika na huduma za kifedha hasa zile za mikopo zenye masharti nafuu na zitakazowawezesha kununua mitambao bora, ambayo itasaidia utendaji kazi kwa ufanisi na ubora zaidi.

Lilian Kitomari(kushoto) wa Stanbic Benki akizungumza wakati wa hafla hiyo, katikati ni
Neimat El Maghraby  Mkuu wa Kitengo cha fedha Mantrac Unatrac Group na kulia ni Adel Selim  meneja wa mantrac Kanda ya Afrika Mashariki.
Akizugumza katika hafla ya kusainiana mkataba huo jijini Dar es salaam hivi karibuni Meneja wa Rasilimali na Bima wa Benki ya Stanbic Tanzania Lilian Kitomari alisema benki yake itaendelea kutoa huduma na njia madhubuti zitakazosaidia wateja wake kutatua matatizo mbalimbali ya kifedha ili kukuza biashara zao nchi nzima.


Meneja wa Mantrac kanda ya Afrika Mashariki Adel Selim akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano ya kibiashara yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Aidha, Rais wa kampuni ya Cat Financial ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Caterpillar Inc, Kent Adams, alisema kuwa “mchanganyiko huo wa bidhaa unaotambuliwa kimataifa kati ya  kampuni ya Cat na Benki ya Stanbic ambazo zinaheshimiwa na kuaminiwa na taasisi za kifedha barani Afrika vitajenga nguvu ya ushindani wenye faida kwa mitandao yetu na wateja wao na kuongeza mauzo yao ya vifaa.”

Naye Naibu Ofisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Standard, Bw. Ben Kruger, alisema “tuna thamini uhusiano wetu uliopo na kampuni ya Cat na tunaamini kuwa uhusiano huu unatoa jukwaa la kuimarisha mahusiano haya na kutoa huduma zaidi kwa nchi nyingine katika bara la Afrika.”

Alisema kuwa Benki ya Standard  Chertered ambayo ni Kampuni mama ya Stanbic Tanzania yenye shughuli zake barani Afrika ina timu ya wataalam ambao ni wazoefu  wa biashara na kanuni, watahakikisha upatikanaji wa huduma bora kwa wateja wa benki hiyo na kampuni ya CAT Financial.
Aliongeza kuwa mpango huo wa magari na rasilimali unafadhiliwa na Benki ya Standard  Chartered ya Afrika Kusini.

Wafanyabiashara hao wa Tanzania wataungana na wenzao wa nchi tano za Nigeria, Kenya Uganda, Ghana na Sierra Leone, ambapo huduma hizo zitatolewa.

Ni kipindi kirefu sasa  Wakandarasi wengi nchini wamekuwa wakilalamikia kukosa mitaji itakayowawezesha kununua mitambo mikubwa na bora ambayo ni chachu ya  kufanya kazi zao kwa ufanisi na ubora zaidi jambo linalowafanya kukosa zabuni mbalimbali za Ujenzi ambazo kampuni za kigeni zimekuwa zikinufaika nazo kwa kuwa na mitambo na mashine za kisasa.


Monday, December 3, 2012

JUAN MATA AKUBALI MADHAIFU YA CHELSEA


London, Uingereza.



MSHAMBUALIAJI wa mabingwa wa Ulaya (Chelsea) Juan Mata amesema kuwa kipigo kikali walichokipata kutoka kwa West Ham cha 3-1 mwishoni mwa wiki iliyopita kilitokana na kupoteza nafasi nyingi walizozipata hasa katika kipindi cha kwanza.


Mhispania huyo aliifungia timu yake bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza kwa kumalizia pasi aliyoipata baada ya kazi nzuri ya Victor Moses na Fernando Torres ambapo bado nafasi nyingi za kufunga zilijitokeza bila kutumiwa.


Mshikanyundo Carlton Cole wa West Ham alipata bao baada ya saa moja na kufanya matokeo kuwa suluhu na baadaye wakaongeza bao mbili na kufanya Mabingwa hao kughalagazwa vibaya.


“Hali ilizidi kuwa mbaya sana kipindi cha pili, kipindi cha kwanza tulipata nafasi za kufunga. Tuliwafunga na tukaongoza kwa muda kipindi cha kwanza” alisema Mata.


Alisema kila mtua aliona kuwa  kipindi cha pili hawakucheza vizuri na kusababisha kupigwa bao tatu na Washikanyundo hao hali iliyosababisha kutoyarudisha mabao hayo kwa haraka.


Mata aliongeza kuwa toka ushindi wao wa mwisho wa Ligi dhidi ya Tottenham Hotspurs katika dimba la Whitepark Lane mwezi October wameambulia  pointi  4 tu dhidi ya 21 walizotakiwa wavune. 


“Inabidi tubadilike na kujiboresha, michezo huwa daima dakika 90 au 95. Tulitarajia  wangetumia nafasi za mipira mirefu ambayo wangepata na walifanya hivyo na kushinda bao la pili” alisema Mata.


Wiki chache za mwisho tumeshuhudia timu yetu ikishuka na kupoteza pointi muhimu, kuna haja ya kubadilika iwapo tunahitajji kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu huu” aliongeza Mata.


Chelsea inazidi kuvurunda kwenye ligi na ligi ya Mabingwa  hasa baada ya kumfukuza kazi kocha aliyewapa mafanikio makubwa msimu uliyepita Roberto Di Matteo mwishoni mwa mwezi uliopita.


Imetayarishwa na Nuzulack Dausen kwa Msaada wa Mtandao.