Madaraka Nyerere atakuwa mgeni rasmi wa maonyesho ya 18 ya Filamu za Afrika (AFF) yanayotarajia kufanyika kuanzia tarehe 29 mwezi mjini Leuven, Ubelgiji. |
Mhe. Dkt. Diodorus Buberwa Kamala, Balozi wa
Tanzania Ubelgiji, Uholanzi, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya anayo furaha
kuwaalika Watanzania wote wanaoishi katika nchi za Ubelgiji, Uholanzi na
Luxembourg kushiriki Tamasha la Filamu za Afrika ambalo litakuwa na siku mbili
maalum za kuonyesha Filamu za Kitanzania.
Filamu ya Kitanzania inayojulikana
kwa jina la “A Teachers Country” itaonyeshwa
tarehe 29/03/2013 katika ukumbi wa sinema wa KINEPOLIS, Bondgenotenlaan
145, Leuven kuanzia saa mbili usiku.
Aidha, tarehe 30/03/2013 Filamu za
Kitanzania zinazojulikana kwa majina ya
“ The Road to Sainthood na Mwalimu: The Legacy of Julius Kambarage
Nyerere” zitaonyeshwa katika ukumbi wa
Museum M, Leuven, Ubelgiji kuanzia saa 5.30 Asubuhi. Mhe. Madaraka Nyerere
atakuwa mgeni rasmi.
Wote mnakaribishwa kuja kushiriki katika
Tamasha la Filamu za Kitanzania.
Imetolewa na Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Balozi wa Tanzania – BENELUX
21/03/2013
No comments:
Post a Comment