Benki ya Akiba Commercial Bank(ACB) imezindua rasmi huduma za
kifedha kupitia simu za mkononi zitakazo wawezesha wateja wa benki hiyo kutuma
na kupokea pesa kupitia mitandao ya simu ya M-pesa, Airtel Money na Tigo pesa.
Akizindua huduma hiyo jijini Dar es salaam jana baada ya kutiliana
saini ya ushirika na Kampuni ya Selcom Wireless, Mkurugenzi Mtendaji wa ACB
John Lwande alisema wateja wa benki hiyo wataweza kutuma na kupokea pesa mahali
popote walipo nchini bila kwenda kwenye tawi la benki.
“Mteja aliyejisajiri na Mobile money ya ACB anaweza kutuma
pesa na kupokea kwa M-pesa kupitia akaunti yake ya simu inayoitwa Mobile Walet.
Pia ataweza kutoa pesa kutoka kwenye akaunti ya ACB na kutuma kwenye akaunti za
Airtel Money na Tigo pesa” alisema Lwande.
Mbali na huduma hizo za kutuma na kupkea pesa, wateja hao
wateweza kurejesha mikopo benki bila kwenda kwenda kwenye tawi la benki na
kupunguza gharama za muda na fedha.
Alizitaja faida za kujiunga na huduma hiyo kuwa ni urahisi wa
kujiunga na kutumia huduma hizo za kifedha zinazopatikana nchi nzima, kutunza
muda na pesa, na pia ni hatua muhimu za kimaendeleo za benki hiyo tangu ilipoanzishwa
mwaka 1997.
Alisema kuwa wateja hao pia wataweza kupata taarifa za salio
la akaunti zao, taarifa fupi za kibenki pamoja na huduma za LUKU, Startimes, na
DSTV.
“Wateja wasiwe na hofu kuhusu suala la usalama tumeshajipanga
kuhakikisha hakuna tatizo katika muamala utakaofanyika kutoka benki kwenda
katika mitandao hiyo na kuleta usumbufu na ikitokea hali hiyo tulishulikia
haraka sana tatizo hilo” alisisitiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa ACB John Lwande(katikati) akibadilishana mkataba na Mkurugenzi mtendaji wa Selcom Wireless Sammer Hirji(kulia) ma kushoto ni Meneja Mkuu wa idara ya ICT wa benki ya ACB. |
No comments:
Post a Comment