Na Nuzulack Dausen
Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal mwishoni mwa wiki iliyopita alizindua rasmi jengo la kuhifadhia mizigo na ofisi za kampuni ya DHL Express (DHL House) lilopo ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikiwa ni moja za jitahada za kampuni
hiyo kurahisa na kuongeza ufanisi katika usafirishaji wa mizigo ya nje na
ndani ya nchi.
Akizindua jengo hilo Dk Bilal alisema ujenzi wa jengo hilo
unaonyesha wazi kuwa DHL imepania kuboresha huduma zake nchini kwa kusafirisha
mizigo mingi na kuhudumia wafanyabiashara wengi zaidi kwa kwa wakati.
Alisema Serikali itaenedela kuboresha miundombinu ili
kutengeneza mazingira rafiki kwa uwekezaji.
Aidha, Bilal aliwataka wawekezaji wote nchini kuiga mfano wa
DHL wa kuajiri asilimia 99 ya wafanyakazi wazawa huku asilimia 40 kati yao
wakiwa wanawake.
Alisema iwapo wawekezaji wataongeza imani kwa wazawa kwa
kuwapa ajira basi tatizo la ajira linalolikumba taifa litatokemezwa na kuongeza
kuwa wataalamu wazawa wapewe kipaumbele katika zabuni mbalimbali jambo litakalo
ongeza tija kwa uchumi na maendeleo ya nchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DHL nchini Braise De Souza alisema
Kampuni yake itaendelea kuboresha huduma zake kwa kiwango cha juu na kuongeza
kuwa wataendelea kuchangia masuala mbalimbali ya maendeleo ya kijamii kama
kutunza mazingira, afya, elimu na kushughulikia masuala mbalimabali ya majanga
ya dharura yanayolikumba taifa.
“Kazi yetu si usafirishaji pekee bali tunasghulikia pia na
masuala ya kijamii kama kusaidia watoto hosptali ya Muhimbili, kutoa ajira kwa
wanawake kwa asilimia nyingi zaidi, ma hivi karibuni tulidhamini tuzo ya Women
of Determination iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu” alibainisha De Douza.
Sherehe hizo za Ufunguzi pia zilihudhuriwa na Waziri wa
Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar
Suleiman Rashidi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said meck Sadiq na wakurugenzi
Viongozi wa Idara mbalimbali za DHL Express wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali waliohudhuria uzinduzi wa jengo la kuhifadhia mizigo na ofisi la DHL Express House. |
Mshindi wa tuzo za Women of Determination Award Nusra Mohamed akiwa na Viongozi waliohudhuria uzinduzi wa DHL Express. |
Mkurugenzi Mtendaji wa DHL Express( kushoto) akimpatia zawadi ya Kifaru Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal(katikati) na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa DSM Said Mecky Sadiq. |
Dk Bilal akionyeshwa kitabu cha DHL EXpress na Mkurugenzi Mtendaji wa DHL Blaise De Souza. |
No comments:
Post a Comment