Nuzulack Dausen
MKAZI wa Tabata Kisukuru Jijini Dar es salaam Mahamoud Said
(22) (pichani juu) anawaomba Wasamaria wema kokote nchini kumsaidia msaada wa fedha
zitakazomsaidia kumalizia gharama za masomo yake.
Said ni mlemavu wa mkono asiyejiweza ambaye amefanikiwa kupata
udahili wa masomo ngazi ya cheti katika Chuo cha Utumishi wa Umma Kilichopo
Jijini Tanga lakini ameshindwa kujiunga mapema na Chuo hicho baada kukosa
fedha.
Anasema kuwa alipata ulemavu wa mkono mwaka 1998 wakati
akicheza mpira ambapo miaka miwili baadaye ulianza kutoa funza ndipo daktari
aliamuru mkono huo kukatwa ili kumnusuru maisha yake.
Ombi hilo linakuja baada ya kupata msaada wa ada kutoka
Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision ambalo lilimsaidia kiasi cha
Shilingi laki nane ambayo inatosheleza kulipia karo kwa mwaka mmoja tu.
Kiwango hicho kilichobaki kinanajumuisha fedha za kujikimu, nauli, sare, vifaa vya kusomea
pamoja na michango yote ya Chuoni.
Awali habari ya kuomba msaada huo ziliandikwa kwenye gazeti la Mwananchi tarehe 27 Novemba
mwaka huu kuhusu ombi la msaada wa kusomeshwa masomo hayo lakini kwa bahati
mbaya hakuna aliyejitokeza kumsaidia, hata hivyo anawaomba wasamaria wema kujitolea
ili aweze kufanikisha masomo yake.
Yeyote mwenye mapenzi mema na mwenye nia ya kumsaidia
tafadhari apige simu au achangie kupitia
M-pesa namba 0766 469 548 au Tigo Pesa namba 0717 511 295.
No comments:
Post a Comment