London,
Uingereza.
MSHAMBUALIAJI
wa mabingwa wa Ulaya (Chelsea) Juan Mata amesema kuwa kipigo kikali
walichokipata kutoka kwa West Ham cha 3-1 mwishoni mwa wiki iliyopita
kilitokana na kupoteza nafasi nyingi walizozipata hasa katika kipindi cha
kwanza.
Mhispania
huyo aliifungia timu yake bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza kwa kumalizia
pasi aliyoipata baada ya kazi nzuri ya Victor Moses na Fernando Torres ambapo
bado nafasi nyingi za kufunga zilijitokeza bila kutumiwa.
Mshikanyundo
Carlton Cole wa West Ham alipata bao baada ya saa moja na kufanya matokeo kuwa
suluhu na baadaye wakaongeza bao mbili na kufanya Mabingwa hao kughalagazwa
vibaya.
“Hali
ilizidi kuwa mbaya sana kipindi cha pili, kipindi cha kwanza tulipata nafasi za
kufunga. Tuliwafunga na tukaongoza kwa muda kipindi cha kwanza” alisema Mata.
Alisema kila
mtua aliona kuwa kipindi cha pili
hawakucheza vizuri na kusababisha kupigwa bao tatu na Washikanyundo hao hali
iliyosababisha kutoyarudisha mabao hayo kwa haraka.
Mata
aliongeza kuwa toka ushindi wao wa mwisho wa Ligi dhidi ya Tottenham Hotspurs katika
dimba la Whitepark Lane mwezi October wameambulia pointi 4 tu dhidi ya 21 walizotakiwa wavune.
“Inabidi
tubadilike na kujiboresha, michezo huwa daima dakika 90 au 95. Tulitarajia wangetumia nafasi za mipira mirefu ambayo
wangepata na walifanya hivyo na kushinda bao la pili” alisema Mata.
Wiki chache
za mwisho tumeshuhudia timu yetu ikishuka na kupoteza pointi muhimu, kuna haja
ya kubadilika iwapo tunahitajji kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu huu” aliongeza
Mata.
Chelsea
inazidi kuvurunda kwenye ligi na ligi ya Mabingwa hasa baada ya kumfukuza kazi kocha aliyewapa
mafanikio makubwa msimu uliyepita Roberto Di Matteo mwishoni mwa mwezi
uliopita.
Imetayarishwa
na Nuzulack Dausen kwa Msaada wa Mtandao.
No comments:
Post a Comment