Nuzulack Dausen
BAADHI ya meneo ya Jiji la Dar es
salaam na Mkoa wa Pwani yanatarajiwa
kukabiliwa na mgao wa maji unaotokana na
uhaba wa huduma hiyo uliyosababishwa na kushuka kwa kiwango cha
uzalishaji wa maji baada ya kuharibika kwa mashine za kusukuma maji katika
mtambo wa Ruvu Juu.
Hayo yamebainishwa na Shirika la
Majisafi na Majitaka la Mkoa wa Dar es salaam( Dawasco) katika taarifa yake
iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana iliyolenga
kuujulisha umma kukabiliana na tatizo hilo.
Taarifa hiyo ilisema maeneo yatakayoathirika
ni Mlandizi, Visiga, Kongowe, Kibaha, Kwa Mathias, Picha ya Ndege, Maili Moja,
Kiluvya, Kibamba, eneo lote la Mbezi, Golani, Kapinga, Mbuzi 40, King’ong’o,
eneo lote la Kimara.
Maeneo mengine ni Changanyikeni,
Ubungo Msewe, Ubungo Kibo, Ubungo Maji, Kilungule, Kibangu, Tanesco, Mandela
Road, Mabibo Hostel, makubuli, Matumbi,
Tabata Bima, tabata Mawenzi, tabata Kimanga, tabata Kisiwani, Kisukuru, Tabata
Chang’ambe na segerea.
“Matengenezo ya mashine hizo
yanaendelea ili huduma ziweze kurudi katika mzunguko wake wa kawaida haraka
iwezekanavyo” ilibainisha taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment