Tuesday, January 22, 2013

MGAO WA MAJI KUWAKUMBA BAADHI YA WAKAZI WA DAR NA PWANI

Nuzulack Dausen

BAADHI ya meneo ya Jiji la Dar es salaam na  Mkoa wa Pwani yanatarajiwa kukabiliwa na mgao wa maji unaotokana na  uhaba wa huduma hiyo uliyosababishwa na kushuka kwa kiwango cha uzalishaji wa maji baada ya kuharibika kwa mashine za kusukuma maji katika mtambo wa Ruvu Juu.

Hayo yamebainishwa na Shirika la Majisafi na Majitaka la Mkoa wa Dar es salaam( Dawasco) katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana  iliyolenga kuujulisha umma kukabiliana na tatizo hilo.

Taarifa hiyo ilisema maeneo yatakayoathirika ni Mlandizi, Visiga, Kongowe, Kibaha, Kwa Mathias, Picha ya Ndege, Maili Moja, Kiluvya, Kibamba, eneo lote la Mbezi, Golani, Kapinga, Mbuzi 40, King’ong’o, eneo lote la Kimara.

Maeneo mengine ni Changanyikeni, Ubungo Msewe, Ubungo Kibo, Ubungo Maji, Kilungule, Kibangu, Tanesco, Mandela Road, Mabibo  Hostel, makubuli, Matumbi, Tabata Bima, tabata Mawenzi, tabata Kimanga, tabata Kisiwani, Kisukuru, Tabata Chang’ambe na segerea.

“Matengenezo ya mashine hizo yanaendelea ili huduma ziweze kurudi katika mzunguko wake wa kawaida haraka iwezekanavyo” ilibainisha taarifa hiyo.

Monday, January 21, 2013

SEKRETARIETI YAANZA KUFANYA UHAKIKI WA MALI NA MADENI YA VIONGOZI WA UMMA

Nuzulack Dausen

WITO umetolewa kwa mwananchi yeyote mwenye taarifa za mali za viongozi wa umma nchini kupeleka taarifa hizo kwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Umma ili kusaidia zoezi la uhakiki wa rasilimali na madeni ya viongozi hao.

 Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inatarajia leo kuanza zoezi la uhakiki wa rasilimali na madeni  ya viongozi wa umma mpaka tarehe 15 februari mwaka huu.

Hayo yamesemwa katika taarifa iliyotolewa mwishoni mwa juma lililopita na Kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda iliyoomba ushirikiano wa karibu kati ya wadau na Sektetarieti katika kukamilisha zoezi hilo.

“Wito unatolewa kwa mwananchi yeyote mwenye taarifa za mali za viongozi hao anaweza kuwasilisha taarifa hizo kwa kamishna wa maadili” alisema Jaji Kaganda.

Zoezi hilo la uhakiki linatarajiwa kufanyika nchi nzima ambapo litahusisha viongozi wote kutoka katika mihimili mitatu ya dola yaani Serikali, Bunge na Mahakama.

 “Wakati wa uhakiki watendaji wa Sekretarieti ya Maadili watatembelea maeneo ziliko mali za viongozi wakiwa na wathamini(valuers) ili kuthamini mali hizo kwa lengo la kujiridhisha na usahihi wa taarifa za mali walizowasilisha kwa Kamishna wa Maadili” alisema Jaji Kaganda.

Alisema taratibu zote za uhakiki wa rasilimali hizo zilishafafanuliwa katika barua za viongozi ambao watahusika katika zoezi hilo awamu hii.

Aidha, Jaji Kaganda aliwatahadharisha viongozi hao kuwaepuka matapeli ambao wanaweza kujifanya ni watendaji wa sekretarieti ya maadili ili kujinufaisha.

“Sekretarieti inawaomba wadau mbalimbali ushirikiano na pia kuwakumbusha kuwa makini na baadhi ya watu wanaoweza kujifanya ni watendaji wa sekretarieti ya Maadili kwa lengo la kujinufaisha” alibainisha Jaji Kaganda.

Aliendelea kusema kuwa endapo viongozi hao watakuwa na mashaka juu ya mwenendo wa mtu yeyote wawasiliane na sekretarieti ya maadili kwa ufafanuzi zaidi.

“Ieleweke wazi kwamba uhakiki ni zoezi la kawaida na watakaohusika na uhakiki huo hawana tuhuma ya aina yeyote ile. Viongozi wanatakiwa kutoa ushirikiano  kwa maafisa wa sekretarieti wa uhakiki huo” aliongeza Jaji Kaganda.

Wednesday, January 9, 2013

WANANCHI WA LINDI NA MTWARA WALIMKOSEA NINI MWENYEZI MUNGU?

Na Nuzulack Dausen
Huu ni Mnara wa Mashujaa uliopo langoni mwa Mji wa Mtwara Mikindani

Itafikia kipindi wananchi wazawa wa mikoa ya Lindi na Mtwara watajiuliza walimkosea nini mwenyezi mungu, kiasi cha kumchukiza na kuwapa laana ya kutokuwa na maendeleo ya haraka kama wananchi wa mikoa  mingine.

Swali hilo linawezekanaa kuwa ni kufuru na dhihaka kwa mwenyezi mungu lakini ni stahili yao kutokana na hali halisi ya maisha wanayoishi pamoja na masahibu yanayowapata wananchi hao wa  mikoa ya kusini kabisa mwa nchi licha ya kujaliwa  rasilimali za kutosha.

Tangu kupata uhuru, wananchi hao wamekuwa wakilalamika kwa kuwa nyuma kimaendeleo baada ya serikali kuwasahau kwa muda mrefu katika mipango mbalimbali ya maendeleo.

Kutokana na hali hiyo wananchi hao waliililia serikali ili iweze kuwatatulia shida zao nao waweze kufikia hatua ambazo mikoa mingine imefikia ambapo serikali ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa iliwafikiria na kuanza kwa kujenga mradi wa barabara kutoka Dar es salaam hadi Mtwara ambayo mpaka sasa haijakamilika.

Hatua za awali zilikuwa ni kujenga daraja katika mto Rufiji maarufu kama daraja la Mkapa ambalo liliweza kuwaunganisha wananchi wa kusini na mikoa mingine ya pwani na Dar es salaam na kuacha kutumia Pantoni.

Pamoja kutatuliwa tatizo la kimuondombinu hususani ujenzi wa barabara ya Dar mpaka Mtwara ambayo bado kilomita chache kukamilika, wananchi wa maeneo hayo bado wanayo ya moyoni ya kutonufaika na mradi wa gesi asili wa Songosongo ambao ulianza miaka 8 iliyopita. 

Licha ya matatizo ya kimiundombinu mikoa hiyo inakabiliwa pia na changamoto za huduma mbaya za afya, elimu, maji, umeme pamoja na ukosefu wa ajira.

Manung’uniko hayo ndiyo yamekuwa chanzo cha mvutano mzito unaoendelea hivi sasa kati ya serikali na wananchi wa Mtwara wakiongozwa na viongozi wa vyama vya siasa huku wananchi hao wakigomea mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam lenye takribani kilomita 532. 

Tukio hilo linaloendelea linazidi kuvuta hisia za watu wa kada mbalimbali nchini tofauti na wakazi wenyewe huku serikali ikiendelea kusisitiza kuendelea na mradi huo kwa madai kuwa rasilimali hiyo ni mali ya taifa na si ya mkoa au kikunndi cha watu fulani.

Kwa mtu ambaye hajawahi kufika mikoa hiyo ya kusini na kuendelea kusikia madai hayo anaweza kuhisi wananchi hao ni wahuni au wahaini kama Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alivyowaita lakini kwa hali halisi mazingira wanayoishi ni magumu yanayohitaji msaada wa haraka.

Kabla mradi huo mpya haujaanza serikali ilibidi ionyeshe kidogo mafanikio ya mradi wa kwanza wa gesi asili kutoka visiwa vya Songosongo ambayo hata Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliyataka.

Sizani Wananchi wote wa Mtwara na baadhi ya watanzania wanaopinga ujenzi wa mradi huo ni vichaa au hawayatakii mema maendeleo ya nchi la ha sha bali wanahitaji kuonjeshwa kidogo namna watakavyonufaika na mradi huo tofauti na miaka ya nyuma.

Wananchi wa Mtwara wameshagutuka kuwa mradi huo unaweza usiwanufaishe sana kama ilivyokuwa kwa ule wa Songosongo. 

Lazima wananchi hao wajiulize kwanini mpaka sasa ni maskini licha baadhi ya wilaya zake kama Nachingwea, Lindi na Mkindani kuwa ni wilaya kongwe nchini kuliko nyingine za mikoa ya Dar esa salaam Kilimanjaro, Mwanza na Arusha ambazo zimeendelea kwa muda mfupi.

Wananchi hao wamegundua kuwa sera ya Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (Corporate Social Responsibility) iliyopo ndani ya rasimu ya sera mpya ya gesi asilia haitawakomboa katika umaskini kama wananchi wenzao waishio karibu na migodi ya madini.

Serikali inapaswa kuyatafakari kwa kina madai ya wananchi hao licha ya kuwa imeshaanza kuugharamia mradi huo. Ni wazi kuwa Serikali haiwezi kuzuiwa kufanya jambo lolote juu ya rasilimali za taifa lakini viongozi wa nchi wakumbuke mvutano huo unaibua hisia tofauti miongoni mwa watanzania ambao ni hatari kwa amani ya nchi.

Mungu hajawalaani wananchi hawa kuwa na maisha magumu na maendeleo finyu ambapo makao makuu ya mikoa yao hayafanani hata kidogo na mitaa ya Tabata Segerea Jijini Dar es salaam au Soweto pale Mbeya Mjini.

Mpaka sasa asilimia kubwa ya wananchi wanaoishi Mtwara mjini katika maeneo ya Magomeni, Ligula, Raha Leo, Mikindani na mengine hawana huduma ya umeme licha ya Serikali kushusha gharama za umeme, hii si kuwa hawajui umuhimu wake bali hawana kipato cha kuwaingizia fedha za kumudu gharama za huduma hiyo.

Vijana wengi hawana ajira, asilimia kubwa za kazi wanazofanya haziwapatii kipato cha kumudu maisha. Licha ya kuwa kuna asilimia kidogo ya ajira katika makampuni yanayotafuata gesi na mafuta mkoani humo  vijana wengi hawana elimu na ujuzi wa kutosha.

Serikali lazima itambue kuwa wananchi wa Lindi na Mtwara hawakulaaniwa na mungu wawe na maendeleo finyu kiasi hicho na pia sera na mipango pendeleo ya nyuma ndiyo chanzo cha matokeo ya umaskini wa maeneo hayo.