Monday, November 26, 2012

WAZIRI WA ULINZI WA ISRAEL ATANGAZA KUJIUZURU




Jerusalem 
Waziri wa Ulinzi wa Irael Barak Ehud akitangaza kujiuzuru kwenye siasa mapema leo hii Jijini Tel Aviv. Picha na AFP

Waziri wa Ulinzi wa Israel Ehud Barak ametangaza kujiuzulu rasmi kwenye Siasa  mapema leo hii Jijini Tel Aviv. Amesema kuwa kujiudhuru huko kutaanza mapema  mwezi Januari mwakani  ili aweze kupata muda mwingi wa kukaa na Familia yake. 

Kujiudhuru kwake kunakufuatia kipindi kigumu kwa Israel ambayo inashuhudia mapigano makali dhidi kundi la Wanangamgambo wa Hamas ambapo siku nane za mapigano wameshauawa watu zaidi ya 160 wengi wao wakiwa ni Wapalestina wa ukanda wa Gaza.

Barak kajiudhuru baada ya kazi ndefu ya Siasa aliyoifanya nchini humo na aliongeza kuwa hata shiriki Uchaguzi ujao utakaofanyika mapema mwezi Januari..




No comments:

Post a Comment