Tuesday, November 27, 2012

FASTJET YAZINDUA RASMI SAFARI ZA NDEGE MIKOANI



KAMPUNI ya ndege ya Fastjet  imezindua rasmi safari zake nchini katika Mikoa mitatu ya Dar es salaam, Mwanza na Kilimanjaro kwa safari mbili za kila siku Dar-Mwanza na Dar-Kilimanjaro na ndege aina ya Airbus A319.  

Afisa Mtendaji wa Fastjet Ed Winter kushoto akiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba wakati wa uzinduzi wa safari ndege za kampuni hiyo.
Akizungumza katika Uzinduzi huo leo Jijini Dar es salaam mgeni rasmi Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba alisema kuwa kuanza kwa safari za ndege za kampuni hiyo inayotoa huduma hiyo kwa bei rahisi kutachangia ukuajiw auchumi kwa kasi sana kwa kuongeza idadi ya Watalii, kutaongeza mzunguko wa biashara na pia kurahisisha safari binafsi za Watanzania.

Tizeba alisema kuwa Serikali inawaunga mkono sekta binafsi hususani katika usafirishaji wa naga kwa kurekebisha Viwanja vilivyopo na kuendelea kuvitengeneza vipya kikiewemo cha Songwe Mbeya kinachotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi desemba Mwaka huu. Aliongeza kuwa kwa sasa wanarekebisha Viwanja Vya Tabora, Kigoma na Mafia huku Kiwanja ch mpada kikiwa kimezinduliwa hivi karibuni.

 Hata hivyo aliitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini(TAA) kuhakiksha inarekebisha miundombinu na huduma za Viwanja vya Mwanza na Kilimanjaro ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya wasafiri watakaotumia Viwanja hivyo.

 Afisa Mtendaji wa Kampuni hiyo Edward Winter alisema kuwa Kampuni yake ina uzoefu mkubwa kufanya biashara hiyo kwa bei nafuu hivyo watanzania wasihofie kushindwa kuendelea kwa kampuni hiyo na kuongez kuwa Safari nyingi zaidi zitaongezwa katika nchi nne za afrika za Kenya, Ghana, Rwanda na Angola.

 Aliongeza kuwa huduma zinazotolewa katika ndege hiyo ni za kisasa na zinazokidhi viwango vya Kimataifa vikiwemo viwango vya Ulaya (European Airline Standards). Hivyo basi Watanzania wachacharikie huduma hiyo ya haraka na bei rahisi kutokea nchini.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Fastjet.

Afisa Mtendaji wa Fastjet Ed Winter akihutubia wadau wakati wa uzinduzi wa safari za  ndege za Kampuni hiyo.

Airbus A319 ya Kampuni ya Fastjet katika picha kabla ya safari ya Uzinduzi mapema leo asubuhi

Maofisa wa Fastjet wakijadilaiana kabla ya ndege Airbus A319 kufanya safari ya Uzinduzi Jijini Dar es salaam

Waandishi wa Habari wakipata maelezo kuhusu safari za ndege za Kampuni ya Fastjet.


Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba kushoto akipewa maelekezo  juu ya ndege ya Airbus A319

Wahudumu wa Fastjet wakiwa katika pozi wakati wa uzinduzi huo.
Safari za ndege hizo zinatarajiwa kuanza mapema keshokutwa Alhamisi ya tarehe 29 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam na gharma yake kuwa ya chini sana ya sh 32000 kwa sfari moja bila kodi sawa na dola 20 za Kimarekani. Hata hivyo gharama za safari hizo zinabadilika pindi muda wa kusafiri unapokaribia.
Hivi ni baadhi ya vitafunwa vinavyopatikana ndani ya ndege ya Fastjet Airbus A319

Watanzania wamehimizwa kuwahi kukata tiketi ili kupata huduma hiyo kwa bei nafuu sana kwani kuchelewa kukata tiketi kutaongeza kiwango cha nauli.

3 comments:

  1. nimesoma habari za ndege za fastjet kwa vyombo vya habari zaidi ya 10 lakini hakuna hata kimoja kilichoeleza ndege inauwezo gani wa kubeba abiria na mizigo kwa safari moja. huu uandishi gani hamuwezi hatu wauliza wahusika maswali kama taarifa fulani haijatolewa

    ReplyDelete
  2. Nimekuelewa ndugu msomaji, kwa taarifa tu ndege hizo aina ya Airbus A319s zinauwezo wa kubeba abiria 175 kila moja. pole kwa usumbufu ulioupata na tunakuhaidi kutorejea makosa kama hayo. Karibu uendelee kusoma habari zetu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Je safari za Kigoma na Tabora bado hazijaanza?

      Delete